Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magufuli, Kenyatta kufungua kituo cha pamoja cha forodha

29661 MALIPO+PIC TanzaniaWeb

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Rais wa Tanzania, John Magufuli na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wanatarajiwa kufungua Kituo cha Forodha cha Pamoja (OSBP) eneo la Namanga upande Kenya na Tanzania kisha kufuatiwa na sherehe ya uzinduzi huo zitakazofanyika upande wa Tanzania.

Viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, wabunge na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wapo upande wa Kenya kwa ajili ya uzinduzi huo unaofanyika leo Jumamosi Desemba 1, 2018.

Lengo la kuanzisha OSBP ni kurahisisha huduma na watu kuchukua muda mfupi kupata huduma za Forodha mpakani.

Kituo cha Forodha cha Namanga ni moja ya vituo vinavyotumika kutoka na kuingia Kenya mkoa wa Arusha, kituo kingine kidogo ni Osmolo kilichopo wilayani Ngorongoro.

 

Endelea kufuatilia Mwananchi



Chanzo: mwananchi.co.tz