Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mageuzi ya kidigitali yashika kasi Zanzibar

Digital Zanzibar.jpeg Mageuzi ya kidigitali yashika kasi Zanzibar

Wed, 13 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Exim Tanzania imesaini Mkataba wa Makubaliano na Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar (eGaz), unaolenga kuendelea kuchochea safari ya mageuzi ya kidijitali.

Makubaliano hayo yametiwa saini baada ya uzinduzi wa hivi karibuni wa Mkakati wa Serikali ya Kidijitali Zanzibar wa mwaka 2023-2027 uliozinduliwa na Dk Hussein Mwinyi, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Akizungumza kabla ya utiaji saini huo uliofanyika visiwani hapa jana, Ofisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya Exim, Shani Kinswaga alisema utiaji saini wa mkataba huo mpya unaendana na malengo ya mageuzi ya kidijitali ya Zanzibar yaliyoainishwa katika Mpango wa Uchumi wa Kidijitali.

Alisema benki hiyo itatumia teknolojia kama dhana ya kutoa huduma za kipekee za kidijitali kwa kushirikiana na eGaz kufanya malipo ya kidigitali ambayo hatimaye yataongeza mapato ya Serikali ya Zanzibar na kuboresha ufanisi.

“Ushirikiano huu mpya unasisitiza dhamira ya benki hiyo kuchangia maendeleo endelevu ya kiuchumi visiwani Zanzibar. Kama benki, tunaamini makubaliano yaliyofikiwa leo sio tu yatachangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi imara, lakini pia yatasaidia kuharakisha mabadiliko ya Zanzibar katika uchumi imara wa kidijitali,” Kinswaga alisema.

Kinswaga alisema mwanzoni mwa mwaka huu, Exim iliboresha mfumo wake na kuweka miundombinu thabiti, hatua inayolenga kuimarisha utendaji kazi wake na kuwapa wateja usalama, ufanisi na uvumbuzi.

“Kama benki, tutaendelea kuwekeza katika teknolojia ili kuongeza uwezo wa mifumo yetuna kutoa huduma bora kwa wateja wetu, jamii inayotuzunguka na taasisi mbalimbali za Serikali visiwani hapa,” Kinswaga alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar (eGaz), Said Seif Said alisema ushirikiano kati ya taasisi hizo ni wa kimkakati na utasaidia kukuza uchumi na kuwezesha ushirikishwaji wa kifedha na kidijitali.

“Huu ni ushirikiano wa aina yake na umekuja kwa wakati muafaka. Tumekuwa tukisubiri wakati huu kwa muda mrefu na tunafurahi tumetia saini makubaliano leo kuashiria mwanzo wa safari yetu ya mabadiliko ya kidijitali,” alisema.

Said alibainisha kuwa taasisi yake itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Benki ya Exim ili kutekeleza mpango wa Uchumi wa Kidijitali wa Zanzibar.

“Tunapoanza safari hii ndefu ya kutekeleza Mkakati wa Serikali ya Dijitali wa miaka mitano, tunafurahi wadau wetu wa kimkakati wamejitokeza kutuunga mkono.

Said aliongeza mabadiliko ya kidijitali ni kipaumbele cha kimkakati kwa Serikali ya Zanzibar na kuongeza kuwa taasisi yake imejipanga kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma za kidigitali kwa kutumia zana mbalimbali za kidijitali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live