Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magereza waongeza uzalishaji Mahindi, alizeti

Wakulima Alzeti Magereza waongeza uzalishaji Mahindi, alizeti

Tue, 7 Feb 2023 Chanzo: mwanachidigital

Jeshi la Magereza mkoani Morogoro linatarajia kuongeza uzalishaji wa mazao ya mahindi na alizeti baada ya kupatikana kwa mtambo mpya wa kisasa unaofanya kazi nne kwa wakati mmoja hivyo kupunguza gharama za uzalishaji.

Akizungumza jana Jumatatu ya Februari 6, 2023 katika eneo la mashamba ya magereza Dakawa wilayani Mvomero, Mkuu wa Magereza mkoani hapa, Kamishna Msaidizi Wilson Rugamba amesema mashine hiyo mpya itaokoa muda, matumizi ya nguvu kazi.

“Magereza tumekuwa tukitumia nguvu kazi watu katika kilimo, lakini sasa baada ya kupatikana kwa huu mtambo nina imani tutazalisha kwa gharama ya chini na bora na hata mazao kuongezeka zaidi,” amesema.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Kilimo, Ndalo Vicent amesema teknolojia hiyo inasaidia kwa kilimo hifadhi na kwa kiwango kikubwa inapunguza gharama za uzalishaji.

“Hii mashine inalima, inapanda na kuweka mbolea pamoja na kupiga haro, hivyo kukata gharama zote,” amesema Vicent.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mzuri Afrika Co Ltd iliyoleta mtambo huo Shaaban Mgonjwa, ameeleza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 41 zinazotumia mtambo huo, duniani, ambapo kwa Afrika ipo na Kenya, akisema utasaidia mazao kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Chanzo: mwanachidigital