Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magari yanayofungwa mfumo wa gesi yaongezeka

Bd9c9bf5babe1afc1e7e7de38585364c Magari yanayofungwa mfumo wa gesi yaongezeka

Sun, 12 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kupanda kwa bei ya mafuta duniani, zaidi ya watanzani 300 kwa mwezi wanabadili mfumo wa magari yao yatumie gesi ikionekana na ongezeko kubwa tofauti na siku za nyuma.

Hayo yamesemwa leo Juni 11, 2022 na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchismi Mramba katika mjadala uliofanyika kwa njia ya Zoom, mada kuu ikiwa ni ‘Mchakato wa Uhamasishaji Matumizi ya Gesi Asilia na Umeme kama mbadala wa nishati ya mafuta kwenye magari.

“ Nimefarijika DIT (Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam) imeanza kubadili magari kwa mwezi yanafika idadi ya magari 300 maana yake kuna mwamko mkubwa wa watu wa kuanza kununua gesi tofauti na siku za nyuma.”Amesema

Mramba amesema serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini ( TPDC), lipo kwenye mchakato wa kuongeza vituo zaidi kwa Dar es salaam -Mtwara -Lindi, vya kujaza gesi asilia kwenye magari yaliyowekewa mfumo huo.

Ametaja maeneo ambayo kutakuwa na vituo vya kujaza gesi ni Kariakoo, Ubungo sehemu yenye kituo cha mabasi, Gongo la Mboto na Mbagala

Amesema Ili kufikia malengo yake ya kuongeza vituo vingi katika maeneo mbalimbali serikali imejipanga kuruhusu na kukubaliana na watu binafsi wenye vituo vya mafuta kuweka gesi kwenye vituo vyao .

“Tangu bei ya mafuta ilivyopanda duniani, nachelea kusema uwezekano wa bei utaendelea kupanda, jumuia ya Ulaya imeweka vikwazo mafuta ya Russia kwa asilimia 70 maana yake zile nchi zimeacha kununua mafuta na hivyo ununua Arabuni ambako tunagombea nazo hivyo 'demand' inaongezeka na gharama lazima ziongezeke, kutokana na hali hiyo watu wengi wamebadili kutoka mafuta ya gari kwa kutumia gesi.

"Gari ya aina yoyote inaweza kubadilishwa mfumo kutoka matumizi ya mafuta na kutumia gesi, na bei yake ni nafuu kuliko bei ya mafuta, unaweza kuokoa zaidi ya nusu ya gharama inayotumika kwenye mafuta." Amesisitiza

Amesema mwekezaji Dangote amebadilisha mfumo wa magari yake yote kwa sasa yanatumia gesi, hivyo wao kama Wizara ili wawe mfano watabadilisha mfumo wa magari yao yote yatumie gesi.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Mhandisi Modestus Lumato, amesema tayari wameanza kuzitembelea karakana ambazo zinabadili mifumo ya magari na kuangalia matatizo yao, na sehemu kubwa ya matatizo yao ni garama za kubadilisha magari kwenda kwenye kutumia gesi kwa kuwa vifaa ni gharama

Amesema EWURA wameanza kuhamasisha watu na kutoa elimu ili watu waelewe umuhimu wa kutumia gesi, na faida zake kwenye magari na hata kwenye kupikia.

“Mitungi TBS ataifuatilia kabla hujaweka kwenye gari lazima ukaguliwe, na kama umeimport mitungi lazima TBS aikague waone kama inafaa kuwekwa kwenye magari.”Amesema Lumato,

Nae, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani, Dk Abdallah Possi amesema gesi imekuwa ni nishati muhimu katika nchi zinazoendelea, mfano Ujerumani karibia robo ya matumizi yote ya nishati yalikuwa ni gesi, mafuta yalikuwa ni asilimia 31.8.

“Yapo magari ambayo yanatengenezwa toka kiwandani kwamba yatatumia gesi lakini ni machache, na sasa naona watu wanahama kutoka kwenye gesi kwenda kwenye betri, sasa je ufundi huo utakuwepo nyumbani?" alihoji na kuongeza

“Ndio tunaweza kutumia gesi kama mbadala kwenye vyombo vyetu vya usafiri, lakini tukiwa tunaelewa kabisa tunakoelekea ni suala la muda kabla nishati ya betri kutumika."Amesema Possi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live