Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magari ya mafuta kupima uzito vituo vitatu tu

9dcc4395fd7efb364f003b394387229e.jpeg Magari ya mafuta kupima uzito vituo vitatu tu

Wed, 15 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Ujenzi imetangaza kuwa kuanzia leo magari yote yanayosafi risha mafuta ndani na nje ya nchi yatapima uzito kwenye vituo vitatu tu ili kupunguza msongamano. Taarifa ya wizara hiyo kwa umma imeeleza kuwa magari yanayoanzia Dar es Salaam hadi Mwanza na Mara yatapima vituo vya Vigwaza, Njuki na Tinde.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, magari yanayoanzia Dar es Salaam hadi Rusumo na Kabanga yatapima vituo vya Vigwaza, Njuki na Mwendakulima. “Vituo ambavyo havikutajwa katika ushoroba wowote havitahusika katika kupima uzito wa magari hayo yanayosafirisha mafuta,” ilieleza taarifa hiyo.

Magari yanayoanzia Dar es Salaam Tabora na Kigoma yatapima katika vituo vya Vigwaza, Itigi na Ilolanguru. “Magari yatakayobainika kuzidi uzito katika mizani inayopima magari yakiwa kwenye mwendo yatalazimika kuingia kwenye kituo husika cha mizani ili kuhakiki uzito,” ilieleza taarifa hiyo.

Magari yanayoanzia Dar es Salaam hadi SongeaRuvuma yatapima vituo vya Vigwaza, Mikumi na Luhimba. Magari yanayoanzia Dar es Salaam hadi Tunduma na Katavi yatapima katika vituo vya Vigwaza, Mikumi na Nkangamo. Magari yanayoanzia Dar es Salaam hadi Mtwara yatapima katika vituo vya Mkuranga, Mingoyo na Ndumbwe. Magari yanayoanzia Dar es Salaam hadi Songea yatapima katika vituo vya Mkuranga, Mingoyo na Sisi kwa Sisi.

Magari yanayoanzia Mtwara hadi Songea yatapima vituo vya Ndumbwe, Mingoyo na Sisi kwa Sisi. Magari yanayoanzia Dar es Salaam hadi Kilimanjaro yatapima katika vituo vya Kunduchi, Msata na Himo. Magari yanayoanzia Dar es Salaam hadi Tanga yatapima katika vituo vya Kunduchi, Msata na Pongwe. Magari yanayoanzia Tanga kwenda Burundi na Rwanda yatapima katika vituo vya Pongwe, Njuki na Nyakahura.

Magari yanayoanzia Tanga kwenda Uganda yatapima katika vituo vya Pongwe, Njuki na Matukula. Magari yanayoenda Malawi kupitia Barabara ya Dar es Salaam, Uyole na Kasumulu yatapima katika vituo vya Vigwaza, Mikumi na Uyole. Magari yanayoenda Zambia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kupitia barabara ya Dar es Salaam- Tunduma yatapima katika vituo vya Vigwaza, Mikumi na Mpemba.

Magari yanayoenda Burundi na Rwanda yatapima katika vituo vya Vigwaza, Njuki na Nyakahura. Magari yanayoenda Uganda yatapima katika vituo vya Vigwaza, Njuki na Kyamyorwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live