Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magari kupimwa uzito yakiwa kwenye mwendo

Serikali Kujenga Mizani Mipya Kudhibiti Uharibifu Wa Barabara Magari kupimwa uzito yakiwa kwenye mwendo

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, ameagiza wataalam wa wizara hiyo kufanya tathmini ya mizani zote nchini na kuangalia bajeti ya kuweka mizani ya kidijitali ya kupima uzito wa magari yakiwa kwenye mwendo (weight in motion), ili iwe katika vipaumbele vya Serikali katika mizani zote ambazo hazijafungwa mfumo huo na zile zitakazojengwa.

Bashungwa ameyasema hayo mkoani Mbeya wakati akikagua kazi zinazoendelea katika mzani wa Uyole uliopo mwanzoni mwa barabara ya Uyole - Kasumulu (mpakani mwa Tanzania na Malawi).

"Dhamira ya Serikali ya kujenga mizani hizo nchini sio kutoza tozo bali ni kujenga utamaduni wa kutozidisha uzito ili kulinda barabara hizo", amesema Bashungwa

Ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu ametoa fedha ya ujenzi wa barabara kuwa njia nne ili kupunguza foleni katika barabara hiyo hivyo ni vema na mizani zitakazokuwepo ziendane na barabara hiyo.

Aidha, Bashungwa ametoa wito kwa wasafirishaji wote nchini kuendelea kuzingatia viwango vya uzito vilivyotolewa kwa ajili ya kutumia barabara zetu ili kuendelea kuzilinda barabara na kuepuka kuingia gharama za tozo za kuzidisha uzito

Naye Mkurugenzi wa Miradi kutoka Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Boniface Mkumbo amesema mzani huo unasaidia kudhibiti magari ya mizigo na ya abiria yanaoenda na yanayotoka Malawi, Kyela na Rungwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live