Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuta yatishia bei ya mchanga, mawe kupanda

25310c2dd7ae3fb9b0a7470dd01bc91f Mafuta yatishia bei ya mchanga, mawe kupanda

Tue, 12 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kupanda kwa gharama ya mafuta ya petroli na dizeli nchini, kumewafanya wafanyabiashara wa mchanga na mawe mjini Geita kuanza kutishia kupandisha bei ya bidhaa hiyo muhimu kwa shughuli za ujenzi.

Akizungumza na Daily News Digital, Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Mchanga mjini Geita, John Fred amesema bei mpya ya petroli imegeuka tishio kwa biashara yao.

Amesema hali hiyo inatokana na ukweli kwamba maeneo ya uchimbaji wa mchanga yapo mbali ya mji, ambapo wanatumia kiwango kikubwa cha mafuta kufuata, hali inayoweza kuwapa hasara wasipopandisha bei.

John amesema kabla ya kupanda kwa bei mpya ya mafuta, bei elekezi kwa roli moja la mchanga, ilikuwa inauzwa kwa wastani wa Sh. 70,000, lakini kwa sasa watapandisha zaidi.

“Kwenye umoja wetu tuna mpango wa kuweka bei halis,i ambayo inaendana na hali ya gharama za uendeshaji, hususani mafuta, ambapo tulikuwa tunahudumia mawe Sh. 80,000 na Sh. 65,000 hadi Sh. 70,000 mchanga, kulingana na maelewano.

“Lakini bei kamili ya mchanga ilikuwa Sh. 70,000 na mawe Sh. 80,000, kwa hiyo kwa ongezeko hili la mafuta, ina maaana lazima tu kufikia Jumatano (kesho) tutakuwa tayari na bei elekezi,” amesema John.

Naye dreva wa roli la mchanga mjini Geita, Nuran Yunus, amekiri changamoto ya bei za mafuta itaathiri gawio wanalopata kutoka kwa wamiliki wa malori, kwani wanapatiwa kulingana na mauzo bila kuzingatia gharama za uendeshaji, ikiwemo mafuta na matengenezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live