Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuta yashuka tena Zanzibar

Mafuta Ya Petrol (1) Mafuta yashuka tena Zanzibar

Fri, 10 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Mapinduzi ya Zanznibar imetangaza kushuka kwa bei ya mafuta ya petroli ikiwa ni muendelezo wa kushuka kwa gharama ya bidhaa hiyo duniani kote.

Mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Maji visiwani humo (ZURA) imetangaza kushuka kwa bei hiyo kwa Sh 100 huku bei ya dizeli, mafuta ya taa na mafuta ya ndege ikisalia kubaki vile vile.

Watumiaji wa huduma hiyo visiwani humo sasa watanunua petroli kwa Sh 2,880 kutoka Sh 2,980 iliyokuwepo mwezi Januari.

"Mabadiliko haya yamezingatia gharama za usafirishaji, kodi ya Serikali, gharama za uagizaji wa mafuta katika bandari ya Dar es Salaam na mwenendo mzima wa mabiliko ya bei duniani" Alisema Afisa mahusiano wa ZURA, Shara Chande Omar.

Kwa watumiaji wa dizeli wataendelea kununua mafuta hayo kwa Sh 2990 kwa kila lita, mafuta ya taa yatauzwa kwa Sh 2681 kama ilivyokuwa mwezi Januari.

Zanzibar inaagiza kiasi cha lita milioni 18 za mafuta kwa kila mwaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live