Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuta ya taa, dizeli yapanda, petroli yashuka

44976 Mafutapic Mafuta ya taa, dizeli yapanda, petroli yashuka

Wed, 6 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Watumiaji wa dizeli na mafuta ya taa nchini watatumia fedha nyingi zaidi kupata bidhaa hiyo mwezi huu huku watumiaji wa petroli wakitabasamu kutokana na mabadiliko ya bei ya ukomo kwa bidhaa za petroli zilizotangazwa leo Jumanne, Machi 5, 2019.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) inaeleza bei ya rejareja kwa dizeli imeongezeka kwa Sh51 kwa lita sawa na ongezeko la asilimia 2.44 na mafuta ya taa Sh50 kwa lita sawa na asilimia 2.47.

Hata hivyo bei ya petroli imepungua kwa Sh23 kwa lita sawa na asilimia 1.07 ikilinganishwa na bei ya mwezi uliopita. Bei hizo zinaanza kutumika rasmi kesho.

“Mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la ndani yanatokana na mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la dunia pamoja na gharama za usafirishaji (BPS Premium),” ilieleza taarifa hiyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz