Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuta mikoa ya Kaskazini kununuliwa Tanga

Mafutapic Mafuta mikoa ya Kaskazini kununuliwa Tanga

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shughuli katika bandari ya Tanga zinatarajiwa kuongezeka kutokana na Serikali kusaini kanuni itakayoelekeza wanunuzi wa mafuta waliopo mikoa ya Kaskazini kununulia mkoani hapa.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dotto Biteko ametoa taarifa hiyo leo, Jumatano Januari 24, 2024 alipotembelea kituo cha kupimia kiwango na ubora wa mafuta ya dizeli, petroli na mafuta ya taa kinachosimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) jijini Tanga.

"Tayari tumeshasaini kanuni tunataka wanunuzi wa mafuta wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini wote wanunulie hapa Tanga na hata wa nchi za jirani tutawashawishi. Tunataka ifikapo Februari utekelezaji uwe unaanza," amesema Biteko.

Meneja wa TPA mkoa wa Tanga, Masoud Mrisha amesema tangu kufungwa kwa mita za kupima mafuta mwaka 2020, Serikali imedhibiti upotevu wa mafuta uliokuwa ukipotea awali na yamebaki na ubora wake

Dk Biteko pia amekagua kituo cha kupokea, kuhifadhi na kusambaza mafuta cha kampuni ya GBP na alielezwa kuwa kina uwezo wa kuhifadhi lita za ujazo 203 milioni na kupakia maroli 12 kwa wakati mmoja kwa dakika 30, huku kikiwa mabehewa 20 kwa dakika 45

Katika ziara yake jijini Tanga, Dk Biteko pia amekagua ujenzi wa Kituo cha kupokea na kulainisha mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda kilichopo Chongoleani ambapo Mkurugenzi wa mradi wa bomba la mafuta la Uganda na Tanga EACOP, Martine Tifen amemweleza kuwa ujenzi umefikia asilimia 35.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live