Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafuta feki yafunga kiwanda Singida

Mafuta Ya Kupikia Mafuta ya Alizeti

Tue, 10 Aug 2021 Chanzo: ippmedia.com

KIWANDA cha kutengeneza mafuta ya kula ya alizeti cha Yaza Investment Company Limited kilichopo mkoani Singida, kimesitisha uzalishaji kwa muda usiofahamika hadi kitakapotatua vikwazo kadhaa.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Yaza, Yusuph Nalompa, wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusiana na kusitisha uzalishaji wa mafuta kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao.

"Wateja wetu na Watanzania kwa ujumla tunawajulisha kwa sasa kampuni yetu haizalishi mafuta ya kupikia ya alizeti yanayotambulika kwa nembo ya “halisi” kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao," alisema Nalompa.

Nalompa alisema mafuta yoyote ya kupikia yanayosambazwa nchini na nje ya nchi yenye nembo ya “halisi” hayajazalishwa na kampuni yao, hivyo wananchi waepukane na matapeli.

“Kama kuna watu wanazalishaji mafuta hayo na kuweka nembo ya ‘Halisi’ ambayo ni mali ya kampuni yetu basi watakuwa wameghushi bila kupata idhini ya mmiliki kinyume cha kifungu cha 32 cha sheria ya biashara na huduma," alisema.

“Tunawaonya wale wote wanaosambaza mafuta hayo kwa kughushi nembo ya “halisi” waache mara moja, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” alisisitiza Nalompa.

Aidha Nalompa amewatahadharisha wateja wao na wananchi kwa ujumla kuwa kampuni yao haitahusika kwa njia yoyote ile na madhara yatakayompata mlaji au muuzaji wa mafuta hayo ambayo hayawazalishi kwa sasa.

Kiwanda hicho kimesitisha uzalishaji huo wakati kukiwa bado kuna ongezeko la bei ya mafuta ya kula katika masoko mbalimbali ya hapa nchini.

Chanzo: ippmedia.com