Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafunzo ya fedha kukuza uchumi nchini

Uchumi Uchumiiii (600 X 300) Mafunzo ya fedha kukuza uchumi nchini

Thu, 17 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Omary Kipanga ametaka mafunzo ya masuala ya fedha kuendelea kutolewa wa wadau wa habari na wadau wa masuala ya fedha na uchumi, ili kuchochea maendeleo ya uchumi nchini.

Naibu Waziri Kipanga ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam, wakati wa mahafali ya mafunzo maalum ya masuala ya fedha yaliyoratibiwa na Bloomberg Media Initiative Africa (BMIA) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwa wadau wa habari na wadau wa masuala ya fedha na uchumi.

Akihutubia katika mahafali hayo Naibu Waziri amehimiza mafunzo haya kuendelea kutolewa kwa waandishi na wadau wa masuala ya fedha wengine kwani yanatija katika kukua kwa uchumi wa Taifa letu. 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live