Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafanikio mkutano wa madini kuiuza Tanzania

Mavunde Rtss.jpeg Mafanikio mkutano wa madini kuiuza Tanzania

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini, Anthony Mvunde amesema mkutano wa sita wa kimataifa wa wakandarasi ni mkutano mkubwa na wa kihistoria kwa sababu ni jambo ambalo halijawahi kutokea Afrika.

Waziri Mvunde amesema hayo leo wakati akihitimisha mkutano wa sita wa kimataifa wa wakandarasi jijini Dar es Salaam

"Nchi yetu Tanzania imepata heshima hii ya kuwa nchi mwenyeji wa mkutano wa sita wa wakandarasi, imetufungua macho ya kuona kwamba zipo fursa nyingine za kuweza kukuza uchumi wetu kupitia madini ya chini ya bahari," amesema Mavunde.

Aidha, amesema jambo hilo ni jipya ambalo Tanzania limekuwa fursa ya kipekee ya kuweza kujifunza na kuelewa rasilimali zilizopo duniani na namna ya kuzivuna kwa ajili ya kuongeza kipato.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live