Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maeneo rasmi ya uzalishaji bado kikwazo kwa wajasiriamali Tanzania

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Lindi. Kukosekana kwa maeneo rasmi ya uzalishaji wa bidhaa mbalimbali za wajasiriamali wa mikoa ya Lindi na Mtwara nchini Tanzania imekuwa kikwazo cha wao kupata alama ya udhibiti wa ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) hivyo kuwa vigumu kuendesha uzalishaji wa wahusika endapo watapatiwa alama hiyo.

Akizungumza jana Jumapili, Agosti 4,2015 katika maonyesho ya nanenane kanda ya kusini yanayofanyika mkoani Lindi, Ofisa kutoka TBS mkoa wa Mtwara, Dinna Lwendo alisema mzalishaji ii aweze kupata alama hiyo anatakiwa kuwa na eneo rasmi ambalo atakuwa anafanyia shughuli za uzalishaji tofauti na shughuli za kawaida za nyumbani.

“Kwa wajasirimali wengi imekuwa kikwazo lakini, tumekuwa tukiwatembelea lakini mazingira tunayokutana nayo ni magumu, mfano wapo wengine wanaotengeneza unga wa karanga wanatwanga kwenye vinu kwa hiyo unaweza kufikiria hali iliyopo.”

“Kwa hiyo inakuwa ni vigumu kuweza kuwapa alama ya ubora kwa sababu ni ngumu kucontrol uzalishaji kwa sababu leo unga unaweza kuonekana mzuri lakini kesho ukawa sio mzuri na ukaleta madhara kwa watumiaji,” amesema Lwendo

Hata hivyo, imeelezwa wajasiriamali wengi wamekuwa hawapeleki bidhaa zao kukaguliwa na hata wanapotembelewa na mamlaka hiyo na kupewa elimu na kusisitizwa umuhimu bado mwitikio unakuwa mdogo.

“Kwanza wanaoleta bidhaa zao wenyewe wao kama wao ni wachache sana, mara nyingi tunawatembelea na kutumia fursa ya mikusanyiko kama haya maonyesho kutoa elimu, lakini  pamoja na maonyesho na kuwasisitizia bado mwitikio ni mdogo mpaka tunapoenda ngazi za juu ili kuweza kufanyiwa kazi kuona ni namna gani wanasaidiwa,” amesema

Pia Soma

 

Mkuu wa wilaya ya Tandahimba, Sebastian Waryuba alisema bidhaa nyingi zimekuwa zikinunuliwa kutoka sehemu mbalimbali na kutumiwa na watu na kutaka mamlaka hiyo kujipambanua na kufikia wajasiriamali ili bidhaa zao ziweze kuuzwa ndani na nje ya Tanzania na kumuondolea hofu mlaji.

“TBS iongeze kasi na nguvu na wigo kuhakikisha wadau wote wanaozalisha wanatembelewa na bidhaa zao kupimwa ili zinapoingia sokoni zisiwe na madhara kwa watumiaji.”

“Mara nyingi bidhaa kama hizi mtu anapokuwa anadhurika anaweza kufungua kesi ya madai, TBS mnaaminika wekeni mazingira ambayo mzalishaji atakuwa na fursa ya kuweza kupata huduma ya TBS kwa sababu bila hivyo wananchi wanaweza kula vyakula ambavyo havina ubora,” alisema Waryuba

Chanzo: mwananchi.co.tz