Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madiwani wavutana ujenzi wa soko

Sikonge Madiwani Madiwani wavutana ujenzi wa soko

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora wameingia katika mvutano mkali wa malumbano ya mapendekezo kuhusu hatua za kuanza kwa ujenzi wa soko jipya la Kariakoo lililopo wilayani humo hatua ambayo imemfanya Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya hiyo Bi. Anna Wilson kususia kikao cha baraza la Madiwani baada ya kuonekana kukerwa na kitendo hicho cha madiwani kuvutana

Mvutano wa kihoja umeibuka wakati baraza hilo maalumu likifanya mapitio ya bajeti ya fedha kwa mwaka 2024/2025 ,ambapo ulizuka mjadala mkali wa wapi ujenzi wa soko hilo uanzie kati ya mazingira ya ndani ama nje ya soko kwa kuanza kuzungushia vibanda

Mwenyekiti wa CCM katika Wilaya hiyo Bi. Anna Wilson alionesha wazi kukerwa na malumbano hayo ya madiwani ndani ya baraza hatua iliyomfanya kusimama kuingilia na baadae kuamua kutoka ndani ya baraza hilo,

Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ya Sikonge Seleman Pandawe nje ya baraza hilo ametoa ufafanuzi wa taswira ya kilichokuwa kikiendelea.

Kando na hilo Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge katika baraza hili imepitisha bajeti ya zaidi ya shilingi Bil.40 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 zaidi bajeti hiyo ikimulika katika kuwapelekea wananchi maendeleo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live