Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Madini yasiwe chanzo uvunjifu wa amani’

Madini Ofii Geita ‘Madini yasiwe chanzo uvunjifu wa amani’

Mon, 4 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Madini, Doto Biteko, amefungua Mkutano wa Wanachama wa Kamati ya Ufuatiliaji na Uchunguzi wa Kampuni zinazohusika na kuchimba madini (ICGLR) kutoka nchi 12 za Maziwa Makuu na kusema wahakikishe makundi ya uchimbaji madini hayahusiki na uvunjifu wa amani.

Biteko amezihakikishia nchi washiriki wa mkutano huo kuwa, Tanzania imeweka mfumo mzuri wa masoko ya kuuza madini, kuchimba na kusimamia kisheria kwa kufuata sheria, ambapo kampuni zinazosafirisha na kuuza madini katika nchi nyingine zinapata vibali vyote vya usafirishaji na hakuna njia za panya.

Alisema lengo la Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo, ni kutokana na kudhibiti vitendo vya utoroshaji madini na uhalifu katika maeneo ya migodi, ambapo kamati hiyo itatembelea baadhi ya masoko ya kuuza madini yaliyoanzishwa na kampuni mbalimbali, ambazo zinajihusisha na kuchimba madini, kusafirisha na kuuza nje ya nchi.

Mwenyekiti wa Kamati ya ICGLR, David Ngoy Luhaka alisema lengo la kamati hiyo ni kuweka uwazi katika masuala ya uchimbaji, ununuzi wa madini, udhibiti utoroshwaji wa madini, kuhakikisha vitendo vya ugaidi havijitokezi kupitia madini na kukemea vitendo vyote haramu vinavyojitokeza kupitia madini.

Alisema kamati hiyo pia itatembelea maeneo yanayochimbwa madini hasa ya Tini huko Kyerwa kwa kuzingatia nchi zote wanachama wanachimba madini ya Tini .

Pia alisema kamati itafanya uchambuzi kwa weledi na kuhakikisha nchi zenye madini zinakuwa chanzo cha amani na kuepusha vita, kuweka uwazi katika uuzaji wa madini, kuhakikisha vikundi vinavyofanya kazi haramu na kuleta machafuko havina nafasi nchi za Maziwa Makuu zinazochimba madini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live