Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madini mapya yagunduliwa songwe

Vibali Madini (600 X 303) Madini mapya yagunduliwa songwe

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo April 17 2023 ameshuhudia utiaji saini wa mikataba ya makubaliano kati ya Serikali na Kampuni tatu za madini kutoka Perth Nchini Australia ambapo amesema Tani milioni 18.5 zenye 4.5% ya madini adimu yamegundulika katika Kijiji cha Ngwala Songwe ambayo yatachimbwa kwa zaidi ya miaka 20.

Akiongea baada ya kushuhudia utiaji saini huo, Ikulu Chamwino Dodoma Rais Samia amesema “kuna maeneo ambayo zamani tulikuwa tunaamini ni masikini sana, hayana rutuba na hayana vyanzo vingine vya fedha, kumbe Mungu ameficha mali huko chini mali ambayo sasa tumejua kwamba ni mali na maeneo yale yanakwenda kunyanyuka”

“Mikoa ya Lindi na Morogoro ipo katika ukanda wa madini Kinywe (Graphite) na Mkoa wa Songwe upo katika ukanda wenye madini adimu "rare earth element" ndio maana miradi hii ipo Chilalo (Lindi), Epanko Wilayani Ulanga na Ngwala wilayani Songwe”

“Hadi sasa kuna kiasi cha mashapo cha tani milioni 67 zenye wastani wa 5.4% ya madini ya Kinywe (Graphite), yaliyogunduliwa katika kijiji cha Chilalo (Lindi) ambayo yatachimbwa kwa zaidi ya miaka 18, Tani milioni 63 zenye wastani wa 7.6 % ya madini ya Kinywe yamegundulika katika eneo la Kijiji cha Epanko ambayo yatachimbwa kwa zaidi ya miaka 18”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live