Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Machinga Kutungiwa sheria

IMG 20220520 WA0021 1080x640 Machinga Kutungiwa sheria

Fri, 20 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula amesema Serikali imeanza mchakato wa kutunga Sheria ya kuwalinda wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama ‘machinga’.

Dkt. Zainab ametoa kauli hiyo jijini Dodoma Mei 19, 2022 wakati akifunga mafunzo kwa viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA).

Katika hatua nyingine Dkt. Chaula ametumia nafasi hiyo kutoa mwezi mmoja kwa mikoa ambayo haijakamilisha usajili wa wanachama wa Shirikisho hilo kufanya hivyo ili kuwepo takwimu sahihi za wanachama zitakazosaidia kuhudumia kundi hilo.

Dkt. Chaula ameongeza kuwa shabaha ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha kundi la machinga linaratibiwa vizuri na linapata fursa mbalimbali za kiuchumi ikiwemo mikopo na masoko ya bidhaa zao.

“Ndio maana Rais Samia akaunda Wizara hii na kuipa jukumu la kuratibu makundi Maalum ikiwepo kundi la Machinga kwa sababu Serikali inawajali na kuwathamini Machinga kama yalivyo Makundi mengine waliopo ndani ya jamii’ alisema Dkt. Chaula

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwemo Shirika la Posta, NSSF, ASAS na wadau wengine waliandaa mafunzo kwa viongozi wa Shirikisho la Umoja wa Machinga nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo katika masuala ya uongozi na kuweka mikakati ya uendeshwaji Shirikisho lao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live