Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabwawa 14 kujengwa kunusuru wakulima

IMG 20221029 WA0080 Mabwawa 14 kujengwa kunusuru wakulima

Mon, 31 Oct 2022 Chanzo: Eatv

Naibu Waziri wa Kilimo, Mh. Anthony Mavunde abainisha mkakati wa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kujenga mabwawa 14 kwa ajili ya kuwezesha kilimo cha umwagiliaji katika mwaka wa fedha 2022/2023. 

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo akiwa Gairo Mkoani Morogoro alipokuwa akifunga maadhimisho ya wiki ya mkulima yaliyoandaliwa na Wilaya ya Gairo.

"Dhamira ya Rais wetu mpendwa, Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kumfanya mkulima kuwa na uhakika na kilimo chake badala ya kutegemea kudra za Mwenyezi Mungu kulima huku akisubiri mvua. 

Na ndiyo maana, ameongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo kutoka bilioni 294 hadi bilioni 954, ambayo kiasi kikubwa imeelekezwa kwenye ujenzi wa mabwawa na miundombinu ya umwagiliaji.

Mabwawa  hayo 14 ni pamoja na, Membe (Chamwino-Dodoma), Msingi (Singida), Kasoli (Simiyu), Katunguru (Mwanza), Iyombo (Tabora), Goweko, Nyida (Shinyanga), Ibanda (Geita), Luiche (Kigoma), Igwisi (Tabora), Kalupale (Tabora), Msagali (Mpwapwa-Dodoma),Mwamabondo na Tlawi (Manyara).

Wizara kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inafanya mapitio ya mabonde yote makubwa nchini yapatayo 22 kwa lengo la kuyafanyia usanifu ili kuwezesha kujenga mabwawa makubwa ya umwagiliaji.

Serikali haipo tayari kuona Mkulima anateseka kuanzia mwanzo anapoandaa mashamba mpaka anapoyauza, ndo maana imeweka mkakati wa kumsaidia katika upatikanaji wa pembejeo na masoko ya mazao anayozalisha.

Chanzo: Eatv