Mradi wa upanuzi na uboreshaji wa miundombinu ya bandari ya Dar es Salaam utakapokamilika, utaongeza uwezo wa bandari hiyo kuhudumia shehena kutoka tani Milioni 17 kwa mwaka hadi kufikia tani Milioni 28 kwa mwaka.
Kauli hiyo imetolewa mkoani Dar es Salaam na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania - (TPA) Ntandu Mathayo wakati wa semina iliyowakutanisha wadau wa shughuli za bandari nchini ili kuwajengea uelewa kuhusu mradi huo.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa gati maalum ya kuhudumia meli kubwa za kitalii, kuboresha miundombinu ya gati la kuhudumia Abiria na mizigo kwa meli za mwambao na ujenzi wa gati mpya nne za kuhudumia Makasha katika bandari ya Dar es Salaam.