Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maboresho bandari ya Bukoba yafika asilimia 38

Bandari Ya Bukoba Maboresho bandari ya Bukoba yafika asilimia 38

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maboresho ya miundombinu katika Bandari ya Bukoba iliyopo mkoani kagera yamefikia asilimia 38 na yanatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu.

Mkuu wa Bandari ya Bukoba, Michael Palangyo amesema shilingi Bilioni 19.5 zimewekezwa kwa ajili ya maboresho hayo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa gati jipya lenye urefu wa mita 100 ambalo litaifanya bandari hiyo kuwa na uwezo wa kuhudumia meli zenye urefu wa mita 92 ikilinganishwa na meli zenye urefu wa mita 75 zinazohudumiwa sasa.

Maboresho mengine yanafanyika katika magati mawili ya zamani, ujenzi wa jengo jipya la kusubiria abiria, eneo la maegesho ya magari na upanuzi wa kina cha maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live