Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maboresho TRC yaongeza mapato asilimia 319

7924a7b80f978dab1aeeb9370a2af540 Maboresho TRC yaongeza mapato asilimia 319

Mon, 8 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema maboresho yanayofanyika katika reli ya kati yamechangia ongezeko la mizigo inayosafirishwa kwa asilimia 232 huku mapato yakiongezeka kwa aslimia 319.

Kadogosa alisema hayo jijini Dodoma alipoezea utekelezaji wa majukumu ya TRC kwa mwaka 2021/2022 na mikakati ya mwaka 2022/23.

Alisema baada ya maboresho ndani ya mwaka mmoja usafirishaji wa shehena za mizigo umeongezeka kutoka tani 186,933 mpaka tani 417,380

Ukarabati huo wa njia umejumuisha kuinua uwezo wa njia kwa kuondoa reli nyepesi na kutandika reli nzito, kuinua uwezo wa madaraja na kuboresha mfumo wa ishara na mawasiliano.

Kadogosa alisema matarajio ya TRC ni kuwa kiwango cha shehena ya mizigo itakayosafirishwa kuanzia kwa mwaka huu wa fedha kuongezeka na kufikia zaidi ya tani 500,000 kiwango ambacho hakijawahi fikiwa kwa miaka 20 iliyopita.

Alisema mapato yameongezeka kutoka Sh bilioni 34 hadi kufikia Sh bilioni 45 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 319.

“Mapato yatokanao na huduma ya usafiri na yale yatokanayo na uwekezaji katika rasimali za shirika ambazo awali zilikuwa kama shamba la bibi, lakini sasa wapangaji wetu wanalipa.”

Alisema TRC pia imelenga kukuboresha maeneo ya upangishaji majengo na maeneo katika jiji la Dodoma na Arusha ili rasilimali hizo ziwe na mchango mkubwa.

Kadogosa alisema shirika limeanza kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa awali wa ujenzi wa reli katika Jiji la Dodoma.

Alisema pia kuna mkakati ili mbali ya Dar es Salaam na Dodoma pia majiji ya Arusha, Mbeya na Mwanza yawe na treni za ndani.

Kadogosa alisema TRC imekamilisha ukarabati wa mabehewa 240 ya mizigo na uundwaji wa vichwa 7 vya Sogeza.

Alisema pia shirika linatarajia kununua mabehewa 22 ya abiria ambayo yanatarajia kuwasili Oktoba mwaka huu.

Kadogosa alisema pia linatarajia kufanya kazi ya uundwaji wa vichwa vitano vya njia kuu na vinve ya sogeza na ukarabati wa mabehewa 37 ya abiria na 600 ya mizigo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live