Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabilioni ya fedha yatumika uzalishaji wa samaki

Samaki Pic Mabilioni ya fedha yatumika uzalishaji wa samaki

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Serikali kwa kutoa fedha zaidi ya Sh bilioni 3.5 kwa ajili ya kupanua uwekezaji katika Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira mkoani Morogoro ili kiongeze uzalishaji wa vifaranga vya samaki hadi kufikia milioni moja kwa mwezi kutoka vifaranga 100,000.

KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Serikali kwa kutoa fedha zaidi ya Sh bilioni 3.5 kwa ajili ya kupanua uwekezaji katika Kituo cha Kuendeleza Ukuzaji Viumbe Maji Kingolwira mkoani Morogoro ili kiongeze uzalishaji wa vifaranga vya samaki hadi kufikia milioni moja kwa mwezi kutoka vifaranga 100,000. Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Florent Kyombo ametoa pongezi hizo wakati kamati hiyo ya kudumu ya bunge ilipotembelea kwenye kituo hicho kilichopo katika Manispaa ya Morogoro. - Kyombo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo na Mbunge wa Jimbo la Nkenge amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi imewezesha na kufanikisha uwekezaji huo mkubwa. - “Tunaipongeza Serikali kwa uwekezaji huu wa Sh bilioni 3.5 zinazotolewa kwa awamu kwa ajili ya mradi wa uzalishaji wa vifaranga vya samaki ambavyo inasambazwa nchini kote ili wananchi kupata lishe na kukuza Uchumi,” amesema Kyombo. - “Sisi tumeliona hili ni jambo jema na umeona kwa macho nah ii ni fursa ya kushauri zaidi kupitia serikali yetu ili kupata kitu chenye thamani kulingana na fedha zilizowekezwa” Amesisitiza Kyombo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live