Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabilioni ya NMB hati fungani kufanya haya...

FEDHA WEB Mabilioni ya NMB hati fungani kufanya haya...

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imeipongeza benki ya NMB kwa kuwa taasisi ya Kifedha ya kwanza Tanzania na Afrika ambayo imeuza hati fungani zake na kupata jumla ya billion 400 fedha ambazo zote zinaelekezwa kwenye utekelezaji wa miradi yenye matokeo chanya kwa jamii.

Aidha benki hiyo ambayo iliuza hati fungani zake zijulikanazo kwa jina la JAMII BOND ndani na nje ya nchi kwa riba ya asilimia 9.5, lengo likiwa ni kukusanya fedha za kitanzania billion 75 lakini hadi dirisha linafungwa mwezi mmoja toka kutangaza kwake jumla ya sh billion 212 .9 zilikuwa zimepatikana sawa na ongezeko la asilimia 284.

Akiongea kwenye hafla ya kutangaza matokeo hayo ya JAMII BOND iliyoingizwa sokoni na benki ya NMB hatua iliyoambatana na uorodheshaji wake kwenye soko la hisa DSE, waziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema matokeo hayo ni ishara muhimu kwa taasisi za kifedha kwamba zinaaminika ndani na nje ya nchi na kwamba uuzaji wa hati fungani hizo za JAMII BOND za benki ya NMB ni utekelezaji wa uchumi jumuishi kwa watanzania.

Kwa upande wake afisa mtendaji mkuu benki ya NMB Ruth Zaipuna amesema fedha zote zilipatikana kwenye uuzaji wa hati fungani ya JAMII BOND zinakwenda kutolewa mikopo yenye matokeo chanya kwenye jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live