Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabenki yaomba msaada urejeshwaji mikopo kwa wakulima

FEDHA Mabenki yaomba msaada urejeshwaji mikopo kwa wakulima

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taasisi za fedha mkoani Mtwara, zimeiomba mamlaka husika kuzisaidia kudai na urejeshwaji madeni sugu yaliyotokana na pesa walizo wakopesha wakulima.

Wawakilishi wa benki hizo wametoa ombi hilo leo wakati wakizungumza katika Mkutano mkuu wa 23 wa Chama Kikuu cha ushirika cha Mtwara Masasi na Nanyumbu, (MAMCU) unaofanyika wilayani Nanyumbu leo Alhamisi Mei 11, 2023.

Meneja huduma na masoko wa Benki ya watu wa Zanzibar, (PBZ), Hamza Mohamed amesema wamekuwa wakitoa mikopo kwa wakulima wa korosho kupitia vyama vya msingi, (AMCOS) vinavyofanya vizuri na wako tayari kuendelea kutoa mikopo.

"Sisi tuko tayari kuhakikisha tunakopesha AMCOS zote lakini wenye mamlaka mtusaidie kudai ikifika muda mnakaa pembeni.

Meneja wa benki ya NMB tawi la Nanyumbu, Shamsi Kashoro kwa niaba ya Meneja wa Kanda ya Kusini yeye amesema kuwa kwa sasa wanatoa mikopo kupitia AMCOS baada ya kuona changamoto kwa mtu mmoja mmoja.

"Kwa muda mrefu sasa tunawadai madeni kiasi kwamba mnatukatisha tamaa, tunaomba ushirika muwaangalie wakulima watumie mikopo vizuri na wafanye marejesho" amesema Kashoro.

Benki zimetoa maelezo hayo kufuatia hoja iliyotolewa na Mbunge wa Nanyumbu, (CCM) Yahya Muhata ambaye amesema kuwa benki haziungi mkono zao la korosho na mengineyo kwa kutokutoa mikopo kwa muda muafaka.

Meneja wa CRDB Kanda ya Kusini, Denis Mwoleka yeye amesema wako tayari kueleza kwanini mikopo haitoki kwa sababu wanafahamu changamoto huko nyuma.

Mwoleka amewataka wakulima kufahamu kuwa wakikopa wanatakiwa kulipa.

Meneja wa Benki ya TCB tawi la Mtwara, Godfrey Banza yeye amekiri kweli changamoto za kurejesha mikopo zipo na walijaribu kufanya tathmini na kugundua kuwa wakopaji wengi hawana elimu ya ujasiriamali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live