Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabasi yote kutoa tiketi kidigitali kuanzia leo

B96103d4330e453ba3b47b0cf0ab2fc3 Mabasi yote kutoa tiketi kidigitali kuanzia leo

Fri, 1 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imesema imejipanga kuhakikisha abiria wote wa mabasi ya mikoani wanatumia tiketi za kielektroniki kuanzia leo.

Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa Barabara wa Mamlaka hiyo, Johansen Kahatano alilieleza HabariLEO jana kuwa abiria wa mabasi wanapaswa kwenda katika ofisi za basi analotaka kusafiria na ataelekezwa namna ya kukata tiketi.

Kwa mujibu wa Latra, kuanzia leo mabasi yote yatatakiwa kutoa tiketi kielektroniki.

“Ili kuepuka usumbufu tuliwafundisha hao wahudumu watakaopokea abiria katika ofisi za mabasi na watakuwa na kifaa cha kukatia tiketi. Nawashauri wananchi wasibabaishwe tena na wapigadebe kwani huduma zote zitapatikana katika ofisi ya basi husika kwa nauli ileile iliyopangwa na serikali bila ongezeko lolote,” alisema Kahatano.

Chama cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA), kimesema mabasi yote yapo tayari kuanza kutoa huduma ya usafiri kwa kutumia tiketi za kielektroniki kama ilivyoelekezwa na serikali.

Mweka Hazina wa Taboa, Issa Nkya alilieleza gazeti hili kuwa hakuna sababu ya mmiliki wa mabasi kukataa au kutojiunga na mfumo wa tiketi za kielektroniki kwa sababu tozo zilizoleta uzito awali ziliondolewa.

cio...

Chanzo: www.tanzaniaweb.live