Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabasi yanayojaza abiria kufutiwa leseni

MABASI MIKOANI Mabasi yanayojaza abiria kufutiwa leseni

Fri, 24 Apr 2020 Chanzo: --

KATIKA kuhakikisha Mkoa wa Tabora, unakabiliana na maambukizi ugonjwa wa corona,umesema utayafutia leseni magari yanayaojaza abiria kupita kiasi.

Agizo hilo, limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Agrrey Mwanri alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa kujadili namna ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Mwanri aliwaagiza wakuu wa wilaya kushirikiana na vyombo vya usalama kuhakikisha magari yatakayokiuka agizo hilo, wamiliki wake wanyang’anywe leseni.

Alisema kuna malalamiko yaliyotolewa na abiria kuwa baadhi ya madereva na makondakta wa magari yanayotoa huduma ya usafiri kutoka wilaya na mkoa huo,hulazimisha kujaza abiria hadi wanasimama ndipo wanaondoa gari kituoni.

Alisema kitendo hicho kinapingana na maagizo na maelekezo yanayotolewa na viongozi na wataalamu wa afya juu ya kujikinga na maambukizi ya corona.

Pia aliwaagiza watendaji kushirikiana na jeshi la polisi kuwakamata wale wote watakaokutwa wakiuza bei kubwa vifaa vinavyotumika kukabiliana na ugonjwa huo.

Chanzo: --