Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabasi ya Mwendokasi kuanza safari Uwanja Sabasaba

28f84a929da010928d11910c96073d24 Mabasi ya Mwendokasi kuanza safari Uwanja Sabasaba

Mon, 6 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara nchini (TANTRADE), imeingia mkataba wa ushirikiano na Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART), utakaowezesha wananchi watakaoenda kutembelea maonesho ya Sabasaba kupata huduma za mabasi hayo.

Wakizungumza wakati wa utiaji saini makubaliano hayo leo, viongozi wakuu wa taasisi hizo, walisema makubaliano hayo kimsingi yanaenda kunufaisha pande zote mbili pamoja na wananchi kwa ujumla.

Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade, Latifa Khamis amesema kupitia ushirikiano huo utakaoanza utekelezaji wake Juni 27 hadi Julai 14 Mwaka huu, wananchi na watu wote watakaoenda kuyatembelea maonesho hayo watatumia usafiri wa mabasi hayo kuanzia kituo cha Gerezani hadi Uwanja wa Sabasaba.

" Hatua hii itawafanya wananchi wote wenye nia ya kuja kutembelea maonesho haya kuondokana na usumbufu wa kukosa usafiri wa uhakika kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na Kibaha," amesema Khamis.

Alisema mbali ushirikiano huo, taasisi hizo mbili pia zimekubaliana kushirikiana katika maeneo mengine ya utoaji huduma mbalimbali ndani ya viwanja hivyo sambamba na kuyatangaza maoneesho hayo kupitia mabasi hayo.

Naye Mtendaji Mkuu wa DART, Edwin Mhede, amesema kuwa kupitia makubaliano hayo, DART itahakikisha kunakuwa na huduma za uhakika kwa watembeleaji wa maonesho hayo.

Amesisitiza kuhakikisha suala hilo linatekelezeka DART imeweka utaratibu wa kuwa na kadi maalumu kwa ajili ya upandaji wa mabasi hayo, hatua ambayo haitomlazimu abiria kukata tiketi mara kwa mara.

"Kwa kuanza na huduma hiyo mabasi yetu yatatumia kituo chetu kilichopo eneo la Mtoni kwa Azizi Ali, kama sehemu yake ya maegesho, huku huduma zikiendelea, kuanzia hapa Sabasaba mabasi hayo yatawapeleka hadi Gerezani mahali ambapo abiria wanaweza kupanda mabasi mengine ya ndani na nje ya mji," amesema Mhede

Chanzo: www.tanzaniaweb.live