Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabasi ambayo hayapo kwenye mfumo wa TRA kufungiwa

Kitumabasipic Data Mabasi ambayo hayapo kwenye mfumo wa TRA kufungiwa

Thu, 15 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imesema wako mbioni kuzifungia kampuni za mabasi zitakazoshindwa kujiunga na mifumo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hadi kufikia Septemba 30, 2022.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Latra, Habibu Suluo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo Alhamisi, Septemba 15, 2022 kuhusu sheria inayotaka mabasi yote ya masafa marefu kujiunga na mfumo wa kutoa tiketi kwa njia ya mtandao.

Suluo amesema sheria inataka mabasi yote ya masafa marefu kujiunga na mfumo wa kutoa tiketi kwa njia ya kimtandao lengo ikiwa kutoa fursa kwa wananchi kukata tiketi mtandaoni popote alipo kwa kuchagua basi na siti anayotaka kukaa kwa kusafiri bila kufuata kituo.

"Pamoja na mfumo huu, nawasihi kampuni za magari na mawakala pia wahakikishe mifumo yao inaunganishwa na mifumo ya TRA, ili kuonyesha tiketi zao ni halali na itafikia mahali tutawaondoa wasiwepo wasipotimiza haya,” amesema

Suluo amesema wanatambua changamoto zinazojitokeza kwenye mfumo huo ikiwemo shida ya mtandao, ambapo wanatarajia kufanya vikao na wadau wa usafiri ili kufanya maboresho ya kutatua tatizo hilo.

"Zipo changamoto ikiwemo ukosefu wa mtandao sehemu nyingi lakini wakati tunatengeneza huu mfumo pia tulitengeneza mfumo jumuishi wa mauzo wa hizi tiketi ili mambo yakisumbua basi abiria wafike pale lakini isiwe ndio mtindo tafadhali," amesema

Pia, wanatoa huduma hizi walipwe maana kuna wanafanya kazi hawalipwi hivyo malalamiko tumepokea na tutakwenda huko mbele kuangalia namna ya kuwadhibiti hawa ili wapate haki yao wasije wakazima hizi mashine zao halafu abiria wakapata shida.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Haki za Watoa Huduma za Mabasi Kanda ya kaskazini, Adolf Masawe amesema mfumo huo umekuwa na mtandao mpana unaosabisha kukwama kwa huduma.

"Kabla ya kuwaza kutufungia, waboreshe mfumo wao ambao haufanyi kazi ipasavyo, waone tutakavyofuata sheria," amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live