Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi kuibeba sekta ya madini

Mabalozi Wa Tanzania Nje Ya Nchi Kuibeba Sekta Ya Madini Mabalozi wa Tanzania nje ya nchi kuibeba sekta ya madini

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo Agosti 30, 2023 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo amewapokea Waheshimiwa Mabalozi Wapya walioteuliwa hivi karibuni kuiwakilisha Tanzania nchini Canada, Namibia, Austria, Oman na Ufaransa jijini Dodoma.

Ziara hiyo ya Mabalozi imelenga kufahamishwa kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini nchini.

Katika kikao hicho Mabalozi watapata taarifa kutoka katika taasisi za Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Taasisi za Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), STAMICO, TEITI na Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC).

Mabalozi hao waliotembelea Wizara ya Madini ni Balozi Joseph Sokoine anayekwenda Canada, Balozi Fatma Rajab- anayekwenda Oman, Balozi Naimi Azizi- anayekwenda Austria, Balozi Ali Jabir Mwadini – anayekwenda Ufaransa na Balozi Ceaser Waitara -anayekwenda Namibia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live