Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabadiliko ya kidijitali sekta za fedha yamkosha gavana BoT

BoT Gavanna.jpeg Mabadiliko ya kidijitali sekta za fedha yamkosha gavana BoT

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Emmanuel Tutuba, amefurahishwa na hatua ambazo sekta ya benki imechukua kuunga mkono juhudi za serikali kukuza ushirikishwaji wa kifedha.

Akizungumza kwenye hafla ya kumkaribisha na kumuaga mtangulizi wake, Prof Florens Luoga, Bw Tutuba alielezea kuridhishwa kwake na maendeleo yaliyofanywa na benki za biashara katika mageuzi yao ya kidijitali.

"Utendaji mzuri wa benki katika mwaka uliopita ni ushuhuda wa mawazo ya kibunifu ambayo benki zimeanzisha ili kuvutia wateja zaidi na kuwapa uzoefu bora," alisema.

"Serikali inatambua kazi nzuri ambayo benki zimekuwa zikifanya katika kufikisha huduma za kifedha kwa Watanzania walio wengi na hivyo kupanua sekta rasmi ya fedha," alisema.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa TBA, Bw. Theobald Sabi , alisema kuwa utendaji kazi wa sekta ya benki ulitokana na ushirikiano ambayo [sekta hiyo] inapata kutoka BoT na juhudi za serikali katika kuweka mazingira mazuri ya biashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live