Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MV Mwanza kuanza kazi Februari 12, 2023

MV Hapa Kazi7b464385623c 780x470 MV Mwanza kuanza kazi Februari 12, 2023

Thu, 9 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meli ya Mv Mwanza Hapa Kazi itashushwa katika maji Jumapili wiki hii kwa ajili ya matengenezo ya mwisho.

Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Eric Hamissi, amesema ujenzi wake umefikia asilimia 82 na kazi zote kubwa zinazohusisha hasa ufungaji wa mashine mbalimbali zimeshakamilika.

Asilimia 18 iliyobaki itahusisha pamoja na mambo mengine, ufungaji wa mitambo ya kuendeshea meli, viti, vitanda, dari, viyoyozi na kupaka rangi.

“Kwa ujumla umbo lote la meli limeshakamilika. Lengo kuu la kushushwa katika maji ni kuangalia uimara wa kazi iliyokwishafanyika, ikiwemo kuchunguza kama kuna sehemu inavujisha,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live