TAARIFA KWA UMMA
Yaoundé, Cameroon, 7 Julai 2022;
Kampuni ya MTN Cameroon ambayo inatekeleza uchambuzi mpya wa taarifa na suluhisho la AI (Artificial Intelligence) linaloendeshwa na LigaData imetangaza kupitishwa kwa azimio la uchambuzi mpya wa data na jukwaa la AI ili kufanikisha uendeshaji mipango yake ya sera ya mabadiliko ya kidijitali.
Suluhisho hili jipya linaunganisha na kuoanisha taarifa za mtoa huduma wa simu na mteja wake kuwa na mwonekano mmoja wa digrii 360 na kuwezesha kufanya maamuzi sahihi kwa wakati, kwa kutumia mfumo wa Data Fabric na bidhaa za Flare za LigaData.
MTN Cameroon inatekeleza uchanganuzi huo ikiwa ni Kampuni ya 13 ya utoaji huduma za simu kutekeleza suluhisho la kiteknolojia la kiubunifu kwa kushirkiana na mshirika wa kimkakati wa data LigaData.
Aidha, Biashara inatarajiwa kuendeleza mafanikio ya OpCos, kutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu zaidi, huduma za pesa kwa simu zilizoboreshwa, kuboresha rasilimali za mtandao na kuboresha uzoefu na utumiaji wa wateja.
Akizungumzia hilo, Reuben Opata, ambaye ni Afisa Mkuu wa Teknolojia na Mifumo ya Habari katika MTN Cameroon amesema Ushirikiano wa kimkakati wa data wa LigaData na MTN Group ulianzishwa mwaka wa 2018.
"Ubia umeona maendeleo makubwa katika kutumia teknolojia mpya ili kusaidia kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati halisi, kuboresha ubora wa taarifa sahihi kwa kiwango kikubwa.
"Kuharakisha ajenda ya nabadiliko ya Kidijiti ya MTN Cameroon ni kipaumbele cha kikuu na utumiaji wa Data ni sehemu muhimu ya dhamira hiyo," Reuben Opata, Afisa Mkuu wa Teknolojia na Mifumo ya Habari katika MTN Cameroon.
"Utekelezaji wa jukwaa letu jipya la data kwa ushirikiano na LigaData hautaleta tu ufanisi wa biashara lakini pia kutoa uzoefu bora wa siku hadi siku kwa wateja wetu waaminifu."
Darya Nasr, Afisa Mkuu wa Mapato katika LigaData, alisema: "MTN Cameroon ina mipango mingi na kabambe ya kutambulisha huduma za kidijitali za kibunifu wa hali ya juu kwa wateja wake.
Tunafurahi kwamba bidhaa na huduma zetu zinaisaidia MTN Kamerun kutumia data na uchanganuzi hata zaidi ili kuunga mkono matarajio yao ya mabadiliko ya kidijitali yanayotokana na data."
www.mtn.cm
www.ligadata.com
Habari hii imesambazwa na Africa Business Communities kwa niaba ya AFRICA
NEWSWIRE
Wasiliana na:
Gregor Cunningham
Meneja wa Programu ya Masoko LigaData
Barua pepe: [email protected]
Kuhusu LigaData
LigaData ya Silicon Valley ni wataalamu wa huduma za data zinazodhibitiwa na bidhaa za watoa huduma za mawasiliano ya simu ili kuwezesha mabadiliko ya kidijitali, kufikia matokeo chanya yanayotokana na data na kuboresha rasilimali za waendeshaji.
Huduma na bidhaa za programu za LigaData hutumiwa na watoa huduma za mitandao ya simu duniani kote kupata thamani kubwa kutoka kwa miundombinu yao iliyopo, iwe kupitia uchanganuzi ulioboreshwa, uamuzi au AI.
Kuhusu MTN Cameroon
MTN Cameroon (MTNC) ni kampuni tanzu ya MTN Group iliyoundwa tarehe 15 Februari 2000, kufuatia kupatikana na MTN International ambayo ni Kampuni ya kwanza ya simu nchini Kamerun, CAMTEL Mobile.
Katika miaka 19 ya kutoa huduma, MTN Cameroon ndiye mtoa huduma kiongozi wa soko la mawasiliano ya kielektroniki nchini Cameroon, na mshirika muhimu wa ukuaji wa kijamii na kiuchumi wa Cameroon.