Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MR. KUKU AZIDI KUSOTA

Mrkuku?fit=800%2C445 MR. KUKU AZIDI KUSOTA

Mon, 24 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Kesi inayomkabili ya uhujumu uchumi mfanyabiashara maarufu, Tariq Machibya(29) maarufu Mr Kuku, imeahirishwa hadi Septemba 7, mwaka huu, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kutokana na upelelezi kutokamilika.

Mshtakiwa huyo anakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 60/2020 ambapo katika mashtaka saba yanayomkabili, ni pamoja na kusimamia na kuendesha biashara haramu ya upatu, kupokea maingizo ya fedha kutoka kwa umma bila kuwa na leseni na mashtaka matano ni kutakatisha fedha.

Inadaiwa kuwa kati ya Januari 2018 na Mei 2020, katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa anadaiwa kusimamia biashara ya upatu.

Pia, Machibya anadaiwa alijihusisha na biashara ya upatu kwa kukubali na kukusanya fedha kutoka kwa umma, akijifanya kwamba watafanya ujasiliamali wa ufugaji wa kuku na wangepata faida ya asilimia 70 ya mtaji wa awali waliowekeza kwa miezi minne na asilimia 90 ya mtaji wa awali waliowekeza kwa kipindi cha miezi sita, kiasi ambacho ni kikubwa katika biashara kuliko mtaji uliokusanywa.

Inadaiwa kati ya Aprili 26, 2019 na Januari 26, 2020 maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, alijihusisha na miamala ya Sh 6.4 bilioni kwa kutoa fedha hizo kutoka katika akaunti inayosomeka kwa jina la Mr Kuku Farmers Ltd iliyopo katika Benki ya CRDB, wakati akijua kuwa fedha hizo ni zao tangulizi la biashara haramu ya upatu.

Pia, anadaiwa kupokea fedha za maingizo ya umma kiasi cha Sh 17 bilioni bila kuwa na leseni. Kesi imeahirishwa hadi Septemba 7, mwaka huu.

Chanzo: zanzibar24.co.tz