Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MICO:Tumieni Bidhaa zenye ithibati halali.

Mico.jpeg Katibu wa MICO Halal Certification Bureau, Sheikh Jumanne Kasonso

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watanzania wameshauriwa kutumia bidhaa zilizopata ithibati ya Halali ili kuepuka madhara ya kiafya wanayoweza kuyapata.

Wito huo ulitolewa Katibu wa MICO Halal Certification Bureau, Sheikh Jumanne Kasonso wakati akizungumzia umuhimu wa bidhaa zenye ithibati ya Halal kwenye ofisi za kampuni hiyo jengo la Butiama Magomeni jijini Dar es Salaam.

MICO ndiyo wakala wa Halal wa Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) ambayo imepata cheti cha kimataifa kwaajili ya kutoa ithibati ya Halal kwa bidhaa zinazotumika nchini na zile zinasafirishwa kwaajili ya kuuzwa nje ya nchi.

“Halal ni kitu kilichoruhusiwa kisheria ambacho hakina madhara kwa binadamu ili bidhaa iwe Halal lazima ikidhi vigezo au viwango vya nchi husika mfano TBS na baada ya kukidhi vigezo hivyo ikidhi pia vigezo vya kisharia (dini), “ alisema

Hivi karibuni MICO International Halal Bureau of Certification ilipata cheti cha kimataifa kitakachoiwezesha kutoa ithibati ya Halal kutoka kampuni ya Hafsa Halal Certification and Food Import and Export Limited ya Uturuki .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live