Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

MADENI: BoT haijalipa Sh3.7bn za wateja

98251 PIC+BOT MADENI: BoT haijalipa Sh3.7bn za wateja

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Sh3.7 bilioni hazijalipwa kwa wateja wa taasisi za fedha zilizofungwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Fedha zilizolipwa mpaka sasa ni Sh7.3 billion sawa na asilimia 66 ya Sh11 bilioni zinazotakiwa kulipwa.

Taasisi hizo saba za fedha kati yake ni benki za wananchi na moja ni benki ya biashara, zilifungwa na BoT kati ya Mei 2017 na Januari 2018.

Benki hizo ni FBME, Mbinga Community, Convenant, Efatha, Meru Community, Njombe Community na Kagera Farmers Cooperative.

Akizungumza wiki hii kaimu mkurugenzi wa Bodi ya Bima za Madeni (DIB), Richard Malisa alisema Sh2.4 bilioni zililipwa kwa wateja wa benki ya FBME.

Malisa alisema Meru wateja wake walilipwa Sh1.4 bilioni na kwamba, benki hizo saba zilikuwa na wateja Sh25,050 ambao bima yao ni Sh1.5 milioni kila mteja.

Pia Soma

Advertisement
Wateja wa Njombe Community walipokea Sh963 milioni, Kagera Farmers Cooperative walilipwa Sh737 milioni, Mbinga Community Sh722 milioni, Covenant Sh570milioni na Efatha Sh472 milioni.

Malisa ambaye ni meneja wa fedha na utawala wa DIB, alikiri kuwapo kwa ucheleweshaji malipo kwa wateja huku wengi wao hasa wa vijijini wakikosa taarifa za madeni yao.

Kuhusu gharama za kufuatilia fedha za benki ya FBME, alisema zilikuwa juu kwa kuwa ilikuwa na hisa nje ya nchi.

Alisema jukumu la DIB lilibaki kuhakikisha wateja wote wanalipwa Sh1.5 milioni kila mteja baada ya benki hizo kufungwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz