Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lumbesa chanzo cha kipato kushuka

Gunia Viazi Lumbesa Lumbesa chanzo cha kipato kushuka

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAKALA wa vipimo mkoani Pwani, imewaonya wafanyabishara kuacha mara moja tabia ya kuendelea kuvunja sheria kwa kutumia vipimo visivyo rasmi ikiwemo rumbesa hatua ambayo itasaidia kuongeza Mapato yao na kuimarisha uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Hayo yalibainishwa na Kaimu Meneja wa wakala wa vipimo mkoani hapa, Hashimu Athuman, wakati akizungumza na wafanyabishara Soko la Loliondo wilayani Kibaha na Bagamoyo, ikiwa ni sehemu ya kuhazimisha sikukuu ya vipimo duniani iliyobebwa na kauli mbiu ya "tupime leo kwa ajili ya kesho endelevu".

Amesema licha ya serikali kutoa elimu na kuwekwa kwa sheria ya vipimo nchini bado baadhi ya wafanyabishara ambao sio waaminifu wamekuwa wakitumia vipimo visivyo rasmi jambo ambalo ni kinyume na sheria na kwamba serikali haita sita kuwachukulia hatua.

"Wafanyabiashara mmekuwa mkitumia visado,ndoo na rumbesa jambo hili halitakiwi ni kinyume cha sheria na mkitumia vipimo hivi mnaweza mkawa mnajipunja wenyewe hivyo mnapaswa kuzingatia sheria mtumie mizani jambo hili litasaidia kuongeza Maputo yenu na ya taifa pia,"amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live