Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lukuvi ashangazwa hali mbaya ya soko

Wed, 19 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tarime. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameuagiza uongozi wa Halmshauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara kuboresha soko la ndizi la Rebu lililopo mjini Tarime ili wafanyabiashara waweze kufanya shughuli zao katika mazingira bora.

Agizo hilo amelitoa mjini hapa leo baada ya kutembelea eneo hilo, ambapo alisema ameshangazwa na hali mbaya ya soko hilo wakati halmashauri imekuwa ikikusanya ushuru kwa wafanyabiashara.

Lukuvi aliitaka halmashauri hiyo kupitia maofisa mipango miji kuboresha soko hilo ili liweze kuwa rafiki kwa wafanyabiashara na wateja.

“Mnakusanya ushuru na hawa watu wanauza ndizi zao chini huku wakichomwa na jua pia hakuna huduma ya maji wala choo hii sio haki kabisa hebu waboresheeni mazingira  kama ambavyo Rais wetu (John Magufuli) anataka kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo" alisema Lukuvi.

Alisema Serikali ipo katika mikakati ya kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wanalipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi, lakini haitafanikiwa kama wafanyabiashara hao hawataboreshewa mazingira ya biashara kama hali ilivyo katika soko hilo.

Naye Mkurugenzi wa Mji wa Tarime, Elias Ntiruhingwa alisema ofisi yake imeomba Sh8 bilioni kutoka wizara ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa la nafaka ambalo litakuwa suluhisho la kudumu juu ya mazingira mabaya ya masomo katika mji huo.

Chanzo: mwananchi.co.tz