Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ludewa kuanza ufugaji samaki

Samaki Ludewa Ludewa kuanza ufugaji samaki

Sat, 22 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la madiwani Wilayani Ludewa mkoani Njombe limepatiwa elimu ya ufugaji samaki kwenye vizimba katika ziwa Nyasa ambapo hivi karibuni wilaya hiyo inatarajia kuanza zoezi la majaribio kwa kizimba kimoja katika kata ya Lupingu.

Akizungumza katika baraza hilo mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Sunday Deogratias amesema alitoa mualiko kwa mtaalamu wa ufugaji samaki kutika katika kampuni ya J &J AGRICULTURE LTD. ili waweze kutoa elimu kwa madiwani hao.

Ameongeza kuwa Halmashauri tayari imejipanga kutekeleza mradi huo ili kukuza uchumi na kuongeza pato la ndani hivyo kupitia madiwani hao wataweza kutoa elimu kwa wananchi kwa ujumla.

Aidha kwa upande wa Ofisa wa uendeshaji na masoko kutoka katika kampuni hiyo Dominick Haule amesema mpaka sasa tayari ameshapata kibali cha kuweka kizimba kata ya Lupingu hivyo ameomba nafasi ya kuweka kizimba kingine katika kata ya Manda.

"Niwaombe watu wa mwambao kufanya utaratibu wa kumiliki maeneo ndani ya maji ikiwemo kuunda vikundi ambavyo vitapewa mafunzo juu ya ufugaji hivyo japo kuna baadhi yatari vimeshapatiwa mafunzo hayo labfa niiombe Halmashauri kuviwezesha vikundi hivyo ili nitakapoweka mimi kizimba na kikundi mojawapo kiweke kizimba jirani yangu", amesema Haule.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live