Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lockdown’ yaathiri asilimia 42.7 ya wafanyabiashara

C7fcbf59f9e6afded06d58ec35e4cffa Lockdown’ yaathiri asilimia 42.7 ya wafanyabiashara

Tue, 1 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAKRIBANI asilimia 42.7 ya wafanyabiashara nchini wamekabiliwa na changamoto kubwa katika ufanyaji wa shughuli zao katika kipindi cha Machi na Aprili, kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona.

Wafanyabiashara hao wameathirika kutokana na serikali kuweka zuio la kukutoka nje (lockdown) ili kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo. Ripoti ya Taasisi ya Takwimu Uganda (UBOS) imeonesha kuwa, takribani asilimia 42.7 ya wafanyabiashara walibainisha gharama za kufanya biashara ni zaidi ya walivyozoea katika kipindi cha Machi na Aprili, mwaka huu.

Lengo la ripoti hiyo ilikuwa ni kuangalia athari za ugonjwa huo katika uchumi wa wafanyabiashara. Mkurugenzi Mtendaji wa UBOS, Chris Mukiza, alisema utafiti huo ulijumuisha sampuli ya wafanyabiashara binafsi 2,377.

Hata hivyo, ni wafanyabiashara 1,182 ndio walitoa majibu UBOS, ambapo nyingine ziliendelea kufanya kazi wakati wa zuio hilo la serikali ikiwa ni asilimia 49.7 ya walengwa.

UBOS ilieleza kuwa, asilimia 75 ya waliofanyiwa utafiti katika sekta za fedha na bima, walieleza gharama kubwa za kufanya biashara katika kipindi hicho na kufuatiwa na sekta ya habari na mawasiliano kwa asilimia 66.4 na usafirishaji asilimia 61.6.

Aprili mwaka huu, Waziri wa Biashara, Amelia Kyambadde, alisema viwanda 4,200 vilifungwa kutokana na zuio hilo la serikali.

Chanzo: habarileo.co.tz