Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Lita Milioni 75 za gesi zasafirishwa kutoka Mtwara kwa mwaka 2016/17

7777 Gesi Mtwara TZW

Fri, 11 May 2018 Chanzo: bongo5.com

Serikali imesema kuwa matumizi ya kusafirisha Bomba la gesi kwa mwaka huu imefika lita za ujazo Milioni 75 kutoka milioni 45 za mwaka 2016/017.



Hayo yamesema na kupitia Naibu Waziri wa nishati Subira Mgalu leo, Mei 10 Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kawe aliyehoji , Bomba la gesi lilijengwa kwa mkopo usiopungua tril 1.5, tulikopa tukajua tunapata suluhu, tunatumia 5% ya gesi, mtuambie bomba la gesi limeishia wapi kuzalisha umeme kwa asilimia zilizobaki 95 nyingine tunaambiwa tena kuwa na Stiglers gorge inaanzia wapi maana naona kama Taifa tunapelekwa tu?

Akijibu swali hilo Mgalu amesema kuwa “Ni kweli serikali ilitekeleza mradi mkubwa huu wa ujenzi wa Bomba la gesi wa mkoa wa Mtwara na kama alivyoeleza kwenye swali lake kwasasa matumizi ya kusafirisha gesi kupitia Bomba hili kwa mwaka huu unaoendelea imefika lita za ujazo Milioni 75 kutaka milioni 45 za mwaka 2016/017 ni wazi ongezeko hili linatokana na maongezeko makubwa naomba nimuhakikishie tulipokuwa tunajenga Bomba hili na ahadi tulizozitoa kwa wana Mtwara ahadi zile ni sahihi kwasababu kuna miradi mbalimbali ambayo inaendelea kwa mfano Mtwara peke yake tunajenga mradi wa kuzalisha umeme wa Megawati 300 kwa kutumia gesi asilia ya mkoa wa Mtwara.”

Aliongeza “Lakini nchi yoyote lazima izalishe umeme kwa kutumia vyanzo mbalimbali huwezi kutumia gesi asilia peke yake ukatosheleza mahitaji ya nchi nzima na ndio maana tunazalisha umeme kwa kutumia maji, tunazalisha umeme kwa kutumia gesi na sasa hivi zaidi ya asilimia 50 Megawati zinazozalishwa zinatumia gesi.”

Alisisitiza kuwa ni wazi kwamba gesi ambayo iligundulika huko Mtwara imeleta tija katika uzalishaji wa umeme lakini kama tunavyofahamu tunavyozalisha umeme kwa kutumia vyanzo vingine, serikali imetafakari kwasababu lengo la serikali ni kuzalisha umeme wa bei nafuu na kumfikia mtumiaji kwa bei nafuu.

Loading...
Chanzo: bongo5.com