Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba amesema Serikali ya Tanzania ilifanya kosa kuingiza jeshi kwenye biashara ya korosho kwani shughuli hiyo ilipaswa kufanywa na sekta binafsi.
Amesema jeshi lina kazi ya kulinda mipaka ya nchi na sio kuhusishwa kwenye masuala ya biashara kwani Serikali inatakiwa kujenga mazingira ya sekta binafsi kuwekeza kwenye shughuli za kibiashara.
Profesa Lipumba ameyasema hayo leo Jumamosi Juni 22,2019 jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la haki na furaha kwa wote lililowakutanisha viongozi na wanachama wa chama hicho.
“Kuna mambo ambayo sekta binafsi inaweza kuyafanya, huna haja ya kupeleka jeshi kwenye biashara ya korosho, mtu anayekutakia mema na kukuheshimu ni anayekueleza ukweli. Hatuna sababu kwa Serikali ambayo haiwekezi vizuri kwenye afya na elimu kuingia kwenye biashara huko inatakiwa kuweka mazingira mazuri,” amesema
“Kazi ya kweli ni kulinda mipaka ya nchi, sio kwenda kununua korosho, tumefanya makosa na sasa tujirekebishe kwa kuhakikisha wakulima waliouza korosho wanalipwa fedha zao, sio kuwarudishia korosho kwamba zimeharibika
Hata hivyo, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mathew Mtigumwe akizungumza na Mwananchi kuhusu hoja hiyo ya Profesa Lipumba alisema jeshi halikuingia kwenye korosho kwa ajili ya kufanya biashara bali kuzikusanya katika sehemu ya usalama huku ikiacha biashara ikifanywa na watu binafsi.
Pia Soma
- Asasi za kiraia Tanzania zaliomba Bunge kuikacha miswada kandamizi
- Makonda aahidi Sh120 milioni kugharamia matibabu ya watoto
- Serikali ya Ireland yaipa Sh1.2 bilioni Repoa
“Sisi ndiyo waanzilishi wa kwanza wa kutetea rasilimali katika nchi hii, sisi sio kazi yetu kupinga kila kitu ndani ya Bunge, mambo ya msingi yote tunaunga mkono kwa sababu yanaleta maslahi mapana kwa watanzania na wananufaika,” amesema
Nachuma ambaye pia ni Mbunge wa Mtwara Mjini amesema, “Kuanzia leo tunazaliwa upya na hatutaki tena kuonewa, wale wote ambao hawaitakii mema CUF ila wako kwa maslahi binafsi watambue kuwa nchi hii ni ya vyama vingi.”