Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Liganga, Mchuchuma bado ni kaa la moto

Liganga Mchuchuma Bungeni (600 X 339) Liganga, Mchuchuma bado ni kaa la moto

Thu, 2 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imelieleza Bunge kuwa hakuna kazi yoyote inayoendelea kwa mujibu wa Mkataba uliosainiwa katika mradi unganishi wa Chuma cha Liganga na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma.

Akiwasilisha taarifa ya Kamati leo Februari Mosi, 2023 Mwenyekiti wa kamati hiyo, David Kihenzile amesema licha ya kusainiwa mikataba katika miradi hiyo lakini inasikitika hakuna kilichofanyika kutokana na sababu za mwekezaji kuhitaji vivutio vya ziada vinavyolenga kumnufaisha zaidi kuliko maslahi ya Taifa letu.

Amesema vivutio vilivyoombwa na Mwekezaji vilikuwa vikikinzana na sheria mbalimbali za nchini. Sheria hizo ni pamoja na Sheria za Kodi, Sheria ya Madini, Sheria ya Rasilimali na Maliasili za Nchi.

Amesema, pia ilibaiinika kuwa Mkataba na Mwekezaji huyo una vipengele kadhaa vyenye mapungufu ambayo yanakinzana na maslahi ya Taifa;

Pia, kucheleweshwa na kuongezeka kwa fidia ya wananchi kutoka Shilingi 11,037,183,020.78 kwa uthamini wa mwaka 2015 hadi Shilingi 15,979,788,649.50 mwaka 2022.

Kihenzile amesema, kiasi hicho kinajumuisha riba itokanayo na kucheleweshwa kwa fidia katika kipindi husika; wakati serikali ikijielekeza katika jitihada za kutafuta mwekezaji mwingine wa kuendeleza mradi, mwekezaji wa awali (SHG) amejitokeza tena na kudai kuwa yupo na ana uwezo wa kutekeleza mradi huo.

“Kuchelewa kwa utekelezaji wa miradi hii takriban miaka 13 kunachelewesha kasi ya maendeleo ya ujenzi wa Viwanda Mama, kushindwa kuongeza thamani ya malighafi za ndani lakini pia kuwakosesha ajira wananchi na kuliingizia Taifa hasara kubwa.”Amesema

Chanzo: www.tanzaniaweb.live