Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Licha ya changamoto kilimo, bado kinasonga mbele – Profesa Nyange

59364 Chagamotopic

Fri, 24 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mratibu wa mradi wa taasisi ya Anspires, Profesa David Nyange amesema sekta ya kilimo inaendelea kusonga mbele na imekuwa na fursa kubwa tofauti na miaka iliyopita.

Profesa Nyange ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Mei 23, 2019 wakati akichangia mada ‘Kilimo, Maisha yetu’ wakati wa mjadala wa Jukwaa la Fikra ulioandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd (MCL) na kuhudhuriwa na Waziri wa Kilimo, Japhet Hassunga.

Amesema miaka ya nyuma ilishuhudiwa mashamba makubwa yaliyowekezwa vizuri yakimilikiwa na wageni wa nje, lakini sasa hivi ni tofauti kwa mashamba ya aina hiyo kumilikiwa wenyeji kwa kulima kilimo cha kisasa.

Profesa Nyange amesema kwa miaka 13 Tanzania imekuwa ikijitosheleza kwa chakula  kutokana na juhudi kubwa zinazofanyika licha ya ukuaji kuwa mdogo.

“Mchango wa sekta ya kilimo imekuwa ikipunguza umasikini na dalili ndio msingi wa mageuzi ya viwanda na uchumi. Hata hivyo, bado tuna changamoto kwenye suala la lishe hasa kwa watoto licha ya kuzalisha kwa wingi,” amesema  Profesa Nyange.

Katika mchango wake, Profesa Nyange amewasisitiza kuhusu umuhimu wa  kilimo cha umwagiliaji akisema bado eneo alijatiliwa mkazo.

Habari zinazohusiana na hii

Chanzo: mwananchi.co.tz