Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leseni za biashara Brela na Halmashauri kwenye mfumo mmoja

Leseni Teess Leseni za biashara Brela na Halmashauri kwenye mfumo mmoja

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali inatarajia kuunganisha mfumo wa utoaji wa leseni za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Tamisemi), hatua itakayofanya leseni zote za biashara nchini kutolewa kupitia mfumo mmoja.

Mfumo huo utahusisha utoaji wa leseni hizo za biashara kupitia njia ya mtandao, lengo likiwa ni kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini na hatimaye kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa sheria Brela inahusika na utoaji wa leseni za Kundi A ambazo ni leseni za biashara za kitaifa na kimataifa, ikiwemo viwanda huku Tamisemi ikihusika na utoaji wa leseni za Kundi B, ambazo ni biashara ambazo hazina sura ya kitaifa na kimataifa.

Akizungumza mjini Musoma leo Jumatatu Juni 26, 2023 katika mafunzo ya siku tatu ya maofisa biashara kutoka katika halmashauri za mikoa 10, Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Leseni za Biashara kutoka Brela, Tawi Kilumile amesema kuwa mchakato wa kuunganisha mfumo huo upo katika hatua nzuri.

"Hadi kufika mwaka wa fedha ujao nadhani mfumo utakuwa tayari na leseni zitakuwa zinatolewa kwa njia ya mtandao, lakini mfahamu kuwa sisi Brela tayari tulianza kutoa leseni zinazotuhusu tangu mwaka 2018 kwa njia ya mtandao,"amesema .

Amesema kuwa yapo mafanikio yaliyopatikana baada ya wao kuanza kutoa leseni kwa njia ya mtanda, ambapo idadi ya leseni zinazotolewa kwa mwaka zimeongezeka kutoka 9,200 mwaka 2018 hadi 14,000 kwa mwaka jana.

"Utoaji wa leseni kwa mfumo mmoja kupitia mtandao una faida nyingi kwa wafanyabiashara na serikali kwa ujumla kwani itasaidia kupatikana kwa takwimu halisi ya biashara zilizopo nchini,pia hii itapunguza gharama kwa wafanyabiadhara pale wanapotaka kukata leseni," amesema Kilumile.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live