Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leseni tano za sikukuu zatoka

31443 Leseni+pic Mabasi ya Mikoani

Thu, 13 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Sakaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imetoa leseni za muda kwa mabasi matano yatakayosafirisha abiria, ili kukabiliana na wingi wa wasafiri kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Hatua hiyo imekuja baada ya kupita siku 23 tangu mkurugenzi mtendaji wa mamlaka hiyo, Giliard Ngewe kuwakaribisha wamiliki wa mabasi yenye uwezo wa kubeba abiria 50 kuomba leseni za muda ili wasafirishe abiria hasa mikoa yenye uhitaji mkubwa.

Akizungumza na gazeti hili jana, ofisa usafiri wa Sumatra, Mohamed Zanda alisema mwitikio wa mabasi umekuwa ni mdogo kwa sababu ya abiria wanaosafiri kujitokeza wachache. “Wamiliki wasitumie shortucut (njia ya mkato), kibali kinatolewa na Sumatra kwa mfumo wa leseni na kwa bei rahisi kuanzia Sh10,000 hadi 32,000 kulingana mahitaji ya wahusika,” alisema.

Wakati huohuo, Kikosi cha Polisi Usalama Barabara kimeendelea na ukaguzi wa mabasi katika kituo cha mabasi cha Ubungo, huku 24 ya kampuni mbalimbali yakizuiwa kwa saa kadhaa baada ya kubainika kuwa hitilafu na dereva moja kushikiliwa kwa uongo.

Miongoni mwa hilafau hizo ni pamoja kukatika kwa ball joint, uchakavu wa matairi na kutofanya kazi kwa ufanisi katika mifumo ya bleki na ukataji kona wa matairi.

Ofisa Mkaguzi Mkuu wa Magari kituoani hapo, Ibrahim Samwix alisema wanakagua magari hayo kwa sababu tatu ambazo ni kuangalia muda wa gari husika, magari mengine yanadaiwa kufungwa vifaa vya malori kinyume cha utaratibu na baadhi ya mafundi wanaotumiwa na wamiliki kukagua magari taalumu zao haziko sahihi.

“ Kitu cha kwanza kinachoweza kusababisha ajali ni uzima wa gari husika na siyo mwendokasi. Uzima wa gari na dereva akiwa katika mwendokasi gari linaweza kumsaidia kupunguza matatizo,

Kwa mujibu wa Samwix, kuna aina tatu za ubovu wa magari ya kwanza ni lile gari linaweza kusababisha ajali, ubovu wa pili ni ule unaosababisha break down na wa tatu ni lile gari ambalo liko mbioni kusababisha ubovu.



Chanzo: mwananchi.co.tz