Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leseni 37 za madini zatolewa

Mavunde Atoa Mwelekeo Mpya Sekta Ya Madini Leseni 37 za madini zatolewa

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Awamu Sita, chini ya uongozi wa Dk. Samia Suluhu Hassan yatekeleza ombi la siku nyingi la wachimbaji wadogo Wilayani Songwe kwa kuwatengea eneo la uchimbaji na kuwakabidhi jumla ya leseni ndogo 37 zilizopo eneo la Kata ya Saza kutoka Leseni hodhi namba RL0009/2014 ya iliyokuwa Kampuni ya Bafex Tanzania Limited.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde alipofika eneo la Saza Wilayani Songwe kukabidhi leseni 19 kwa wachimbaji wadogo wa Kikundi cha Songwe Gold Family (SGF) na wachimbaji wengine wadogo wadogo 18 huku mchakato wa kuendelea kutoa Leseni zaidi ukiendelea.

"Nimefika hapa leo kwa maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye amenielekeza nije kuwakabidhi leseni zenu za wachimbaji wadogo mlizomuomba na kuwa mnakwenda kuwekeza mitaji mikubwa sasa na kuongeza mzunguko wa fedha zitokanazo na shughuli za madini kufikia zaidi ya Trilioni moja.

Pamoja na kwamba mnachimba kwa kubahatisha, kwa kipindi cha Julai, 2023 hadi Februari, 2024 mmezalisha kilo 729.6 zenye thamani ya bilioni 101.06, ninaamini kwa kupatiwa leseni hizi hamtakwenda kumwangusha Rais Samia kwa kuongeza uzalishaji na mapato yatokanayo na madini.

Pia, Waziri Mavunde alibainisha kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha inaondoa ujanja ujanja kwenye shughuli za uchimbaji madini ambapo tayari ameshatangaza kufuta jumla ya leseni na maombi 2648 ambazo hazijaendelezwa na zimekiuka taratibu za umiliki wa leseni za madini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live