Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Leseni 200 za madini zafutwa

Madini Ofii Geita Leseni 200 za madini zafutwa

Fri, 29 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

 Jumla ya leseni 200 za uchimbaji wa madini zimefutwa huku taratibu za kufuta zingine 400 zikiendelea.

Takwimu hizo zimetolewa leo Ijumaa Aprili 29, 2022 na Waziri wa Madini, Dk Doto Biteko wakati akitoa ufafanuzi kwa wabunge kwenye hitimisho la hoja yake ya kuomba makadilio ya mapato na matumizi ya mwaka 2022/23.

Dk Biteko amesema leseni hizo ni zile ambazo hazikufuata taratibu na sheria za uchimbaji wa madini hivyo kuwa zimekosa uhalali wake.

Amesema leseni nyingi zinachukuliwa kwa mtindo wa kutegesha hivyo kuwa leseni tegesha ambazo mwisho wake hazina tija kwa nchi.

Hata hivyo Waziri amesema kazi ya usimamizi wa madini ina lawama kubwa hivyo inahitaji maamuzi kwa manufaa ya wananchi huku akieleza kuwa kazi ya kuwalinda wachimbaji wadogo itaendelea.

Amesema shughuli nyingi za madini zinazofanywa kinyume na utaratibu, hazitavumiliwa lakini ulinzi kwa wanaofuata sheria itakuwa ni jukumu la Serikali.

Advertisement Katika hatua nyingine Spika ameonya kwa Mawaziri kuacha kuteua mabalozi wa Wizara zao kwa kufuata upendo na kujuana kwani kila mmoja akifanya hivyo haitakuwa na maana.

Kauli ya Spika imekuja baada ya Waziri kuwateua mabalozi wa madini Jane Jelly, Munde Tambwe, Asia Halamga, Stella Manyanya na Ritta Kabati.

Amesema haina maana ikiwa Mawaziri watakuwa wanafanya kazi ya uteuzi bila kuangalia anayeteuliwa ni nani na anasifa zipi za kufaa kuifanya kazi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live