Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Latra yahimiza mabasi tiketi za kielektroniki

225d377fec033f15896256ec68ec51ec Latra yahimiza mabasi tiketi za kielektroniki

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Udhibiti Usafi ri wa Ardhini (Latra) mkoani Tabora imezitaka kampuni za mabasi zinazotoa huduma za usafi ri wa abiria mkoani humo kujiunga na mfumo wa kielektroniki na kuanza kutoa tiketi za mtandao ili kudhibiti upotevu wa mapato.

Ofisa Mfawidhi wa Latra mkoani hapa, Nelson Mmari, alitoa mwito huo wakati akizungumza na HabariLEO kuhusu mfumo huo wa utoaji tiketi ulioanza kutumika mkoani hapa Januari 25 mwaka huu.

Alisema wataanza na kampuni zinazotoa huduma za usafiri kutoka Tabora-Dar es Salaam, TaboraMorogoro, Tabora-Dodoma na Tabora-Mbeya ambapo hadi sasa Kampuni ya mabasi ya NBS ndiyo imeingia kwenye mfumo huo.

Kwa mujibu wa Mmari, abiria anayehitaji kusafiri kupitia njia hizo, anapaswa kukata tiketi kupitia mtandao kwa kuangalia kampuni za mabasi, njia za safari, orodha ya mabasi na kuchagua basi analohitaji kupitia simu yake ya mkononi na kuchagua nafasi.

Alisema namna ya kupata tiketi hizi ni kwenda katika ofisi za kampuni za mabasi kwani zote zinatakiwa kuwa na mashine za kielektroniki (POS) ili kutolea tiketi hizi.

“Namna nyingine ni kukata tiketi hizo kwa kutumia mashine zitakazokuwa zinatumika ndani ya mabasi kwa abiria wapandao njiani,” alisema.

Alisema mfumo huo ni rahisi kwa kuwa unamwezesha abiria kuona mabasi yote kupitia simu yake ya mkononi ili kuona idadi ya kampuni za mabasi zilizopo, kuchagua basi analohitaji na kufanya malipo hapo hapo kwenye mtandao.

“Mfumo huo unaondoa usumbufu waliokuwa wakipata abiria kutoka kwa mawakala wa mabasi na hata inapotokea mtandao kukatika, mteja atatakiwa kusubiri kidogo hadi utakaporudi ili kuchukua tiketi yake … Mabasi yatakayoshindwa kujiunga na mfumo hayataruhusiwa kupakia abiria,” alisema Mmari.

Alisema faida nyingine zitokanazo na huduma hizo ni pamoja na kumpa uhuru mteja kuchagua gari na kiti anachopenda na malipo ya nauli kumfikia moja kwa moja mmiliki wa gari.

“Faida nyingine ni wamiliki wa kampuni kupunguza gharama za uendeshaji biashara, kusaidia kupima tija ya uendeshaji biashara, serikali kupata takwimu sahihi na kwa wakati za mapato, idadi ya mabasi na idadi ya abiria waliosafirishwa,” alisema.

Akaongeza: “Nauli za mabasi zinazowekwa kisheria hazipaswi kupunguzwa kwa zaidi ya asilimia 10 ili kuepusha uwezekano wa kuua biashara ya magari mengine na haipaswi kuongezwa kupita kiwango kilichowekwa kisheria kwa kuwa kitamuumiza abiria.”

Kwa mujibu wa Mmmari, elimu mintarafu huduma hizo zitaendelea kutolewa na Latra, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Jeshi la Polisi kupitia njia mbalimbali vikiwamo vyombo vya habari, matangazo ya ndani ya vituo vya mabasi na ndani ya mabasi yenyewe.

Alitaja kampuni zilizoidhinishwa na Latra kusajili mabasi ili kujiunga na mfumo huo wa utoaji huduma kuwa ni Jetsafari, TINGG, My Safari, Bus Bora, Safasi Online, Msafiri, OTAPP, Safasi Yetu, Bus Ticket na Tiketi Mkomboz

Chanzo: habarileo.co.tz