Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Latra yabaini madereva kupandisha nauli, Waziri Kamwelwe ataja suluhisho

89659 USAFIRI+PIC Latra yabaini madereva kupandisha nauli, Waziri Kamwelwe ataja suluhisho

Tue, 24 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (latra) Gilliad Ngewe amesema wapo baadhi ya wenye mabasi wamekuwa wakilazimisha abiri kuongeza nauli wakiwa njiani.

Ngewe ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Desemba 23, 2019 mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe aliyefika kituo kikuu cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam kujionea hali ilivyo.

Amesema baada ya madereva kubanwa kituoni hapo wapo ambao wamekuwa wakilazimisha abiria kuongeza nauli wakiwa njiani.

“Upo ujanja mwingine tumebaini baada ya hali kuwa shwari Ubungo, madereva wengine wasiokuwa waaminifu tumebaini wakiwalazimisha abiri kuongeza nauli wakiwa njiani,” amesema Ngewe

“Kwa sasa tumeshawagundua vijana wetu wako kila mahali ukifanya Chalinze tutakukamata Msata au Korogwe,” amesema

Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema ulanguzi unaofanyika hata fedha zinazopatikana haziendi kwa wamiliki wa mabasi hivyo kuna haja yakuanzisha tiketi za kielektroniki.

Amesema hali ya usafiri kati kituo hicho kwa mwaka huu imekuwa tofauti na miaka mingine kwani kuna utulivu tofauti na miaka mingine iliyopita.

“Nikiri kwamba mwaka huu kuna utulivu ingawa jana na leo abiria wameongezeka ustaarabu na utulivu” amesema Waziri Kamwelwe

Amesema juhudi za kufufua treni zimesaidia kupunguza msongamano wa abiria kituoni hapo.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz